Mtendaji Mkuu DSE akutana na Waziri wa Fedha

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salam (DSE) aliyefika kujitambulisha. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Dkt. Nchemba, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Bw. Peter Nalitolela, (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka DSE baada ya Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE kujitambulisha kwa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha).

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Bw. Peter Nalitolela, aliyefika kujitambulisha, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *