NA TULLO CHAMBO, RT
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), unatarajiwa kufanyika Juni mwaka ahuu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Katibu Katibu Mkuu wa RT, Wakili Jackson Ndaweka, awali ilitarajiwa uchaguzi ufanyike ndani ya Aprili, lakini kwa sababu zisizozuilika unalazimika kufanyika tarehe za mwanzoni za mwezi wa sita.

Wakili Ndaweka, alibainisha kuwa taarifa rasmi na ratiba ya matukio kuelekea uchaguzi huo, ambayo yataanza ndani ya Mei, itatolewa wiki ijayo kabla ya Ijumaa.
Wakati huo huo, Wakili Ndaweka alisema Mashindano ya Afrika ya Vijana chini ya miaka 18 na 20 yaliyokuwa yafanyike nchini Algeria, sasa yamehamishiwa Nigeri
“Vilevile tarehe za mashindano zimesogezwa mbele kutoka tarehe 14-18 Julai 2025 na sasa yatafanyika Tarehe 16-20 Julai 2025.
Hii ni kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi kama ilivyoelezwa na Rais wa Shirikisho la Riadha Afrika CAA ndugu Hemed Kalkaba Malboum,” alisema Wakili Ndaweka na kuongeza.
Taarifa ya awali ni kwamba, tunatarajia kuwa na mashindano ya majaribio mnamo Juni 8, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua timu ya Taifa itakayowakilisha nchi katika mashindano haya.