Kampuni Hayles ilipewa Jukumu la Usafi kwa kushirikiana na Kikosi cha JKU na KMKM katika maeneo ya Mkoa wa Mjini Magharibi wameziomba Baadhi ya Taasisi za Serikali kuzipa mashirikiano katika kuhakikisha jukumu walilopewa na Serikali la Usafi linaweza kufanikiwa kwa Ufanisi.
Akizungumza wakati wa Usafi katika maeneo ya Barabara na Pembezoni mwa Nyumba za Michenzani Meneja Mkuu Kampuni Hayles Tanzania Allan Suod Wekesa amesema zipo baadhi ya Taasisi zinapashwa kutoa mashirikiano ikiwemo Shirika la Nyumba na Mamlaka ya Maji Zawa kwani maeneo hayo kumekuwa na tatizo kubwa na uvujaji wa maji pamoja na kufurika kwa makaro.
Ameeleza kuwa maeneo hayo yamekuwa yakituwama maji machafu ambayo hutiririshwa kutoka katika nyumba hizo za michenzani pamoja na baadhi miundombinu ya maji kuvunja jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa Afya za Wakaazi wa Maeneo hayo.
Aidha amewaomba wananchi wanaoishi katika Nyumba za Michenzani kuendelea kushirikiana na kikosi kazi hicho kilichopewa kazi ya Usafi na kuhakikisha wanaimarisha Usafi katika maeneo yanayowazunguka.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa Bi Zainab Khamis Kibwana Amesema Maeneo hayo yamekuwa na Changamoto kubwa ya uwepo wa maji machafu pamoja na kuegeshwa Magari Pembezoni mwa Barabara hivyo watahakikisha wanaungana kwa pamoja na Taasisi zainazohusika katika kuondoa changamoto hizo.
Sheha wa Shehia ya Kisima Majongoo Jackob Jackob Mwakengele amesema hali ya maeneo hayo ni mbaya hivyo ni vyema kwa Serikali kusaidia katika Eneo hilo kutokana na changamoto kuwa kubwa jambo ambalo wananchi pekee hawatoweza kukabiliana nayo.