RAIS MWINYI: SMZ ITAENDELEA KUIIMARISHA SEKTA YA ELIMU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali vu Mwinyi amesema Serikali itaendelea Kuimarisha Miundombinu ya Sekta ya Elimu kwani ndio Kipaumbele cha kwanza cha Serikali anayoiongoza.

Rais DktMwinyi amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Skuli Tatu Mpya za Msingi za Ghorofa za Chumbuni, Kidichi na Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume iliopo Mwera.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inajikita Kuimarisha Sekta ya Elimu kuanzia ngazi ya Msingi , Sekondari na Vyuo Viikuu kwani ni nyenzo Muhimu ya kufanikisha Maendeleo katika Sekta zote.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea na Ujenzi wa Skuli za ghorofa katika maeneo mbalimbali pamoja na Kuongeza Idadi ya Walimu sambamba na Kuimarisha Maslahi Yao ili watekeleze Majukumu Yao kwa Ufanisi zaidi.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inakusudia kuzifanya Skuli zote kuwa na Viwango Bora vya kujifunzia kwa kuwa na Vifaa vya kutosha vya kujifunzia, Maabara, Maktaba na Vyumba vya Kompyuta Ili kuwaandaa Wanafunzi katika ngazi za awali.

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Muhammed Mussa amesema Mageuzi Makubwa yanayoendelea katika Sekta ya Elimu yanasaidia Kuongeza Ufanisi katika Utekelezaji wa Mtaala Mpya wa Elimu na Ongezeko la Ufaulu wa Wanafunzi.

Akiwasilisha Taarifa ya Kitaaluma ya Ujenzi wa Skuli hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khamis Abdalla amesema kila Skuli imegharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 4.5 hadi kukamilika zikiwa na Madarasa 29 kila Moja , Maabara, Maktaba na Vyumba vya Kompyuta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *