
Wana Tipi Lindanda Pamba Jiji FC leo wana kibarua kizito dhidi ya Mabingwa watetezi Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL Yanga SC katika Dimba la Kirumba jijini Mwanza kuanzia majira ya saa 10:15 jioni.
Ni mchezo ambao umebeba taswira tofauti kutokana na mambo mablimbali yanayoendela nje ya Uwanja na kufanya wapenzi wa Soka kutaka kushuhudia kitakachjiri miamba hiyo miwili itakapomenyana kuzisaka alama tatu.
Yanga wanahitaji ushindi kuendelea kujikita katika kilele cha msimamo wa NBC PL ambapo ni mchezo wao wa 22 msimu huu na kuzidi kuwapa presha wapinzani wao Simba SC ambao wanafukuzana kuusaka uchampioni msimu huu.
