Rais Dk. Samia amsamehe January Makamba hadharani

MIEZI Saba tangu alipomuondoa kwenye nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametangaza kumsamehe na mkumrejesha kwake Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba.

Julai 21 mwaka jana, Rais Samia alimuondoa Makamba madarakani na nafasi yake kujazwa na George Simbachawene, lakini leo akiwa ziarani Lushoto mkoani Tanga, Rais Samia ambaye awali hakutaja sababu za kumuondoa wizarani, ametangaza kumsamehe.

“Nihitimishe kwa kuwashukuru Wananchi wa Lushoto kwa mapokezi mazuri na nataka niseme bado nipo Tanga na wiki yote hii ni ya Tanga.

“Lakini mwisho kabisa nataka nimwite mwanangu January hapa aje, arudi kwa mama. Sisi wamama mnatujua… ukimkera mama anakupiga kikofi anakufichia chakula.

“Sasa mwanangu nilimpiga kikofi nikamfichia chakula, si ndio…lakini leo ninamrudisha kwa mama,” alisema Rais Samia na kumkumbatia Makamba, mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, Yusuph Makamba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *