Timu ya Taifa ya ngumi kwa upande wa wanawake imeingia rasmi kambini jana na kuanza mazoezi kwa mtindo wa kwenda na kurudu yani nyumbani mpaka watakapopata kambi rasmi.
Mwenyekiti wa kamati ya wachezaji na wanawake wa shirikisho la ngumi la Taifa BFT, Aisha George amesema kwa sasa timu hiyo ya Taifa inafanyia mazoezi katika chuo cha polisi kilwa road kilichopo kurasini jijini Dar es salaam kwaajili ya kujiandaa na mashindano ya ubingwa wa Dunia yatakayofanyika mwezi Machi mwaka huu nchini Serbia.
Aisha amesema timu hiyo inakabiliwa na ukata kiasi ambacho hadi sasa hwajapata kambi maalum, hakuna tiketi za ndege za mabondia, bima kwa mabindia, gharama za chakula na maandalizi mengine ya mahali watakapofikia huko nchini Serbia endapo wakifanikiwa.
Shirikisho hilo la ngumi la taifa linawaomba wadau kujitolea kuwasaidia mabondia hao wakike watakaoenda kuipeperusha bendera ya Tanzania huko nchini Serbia ili kulinda heshima ya nchi yetu katika mchezo wa ngumi.
Endapo ukiguswa na ukitaka kujua namna ya kuisaidia timu hiyo ya Taifa basi wasiliana nao kupitia namba hizi za simu ya mkononi +255713106683.
