Kuna watu huwa mabingwa wa kuwapiga matukio wenza wao.Lakini kupitia ujumbe huu ninakupa guarantee kwa 100% kama utazingatia maelekezo ya ujumbe huu kamwe hauwezi kupitia maumivu ya mapenzi baada ya kufanyia kazi.
Mara kadhaa tumeona matukio ya aina hiyo
I.MWANAUME MWENYE HURUMA KUPITILIZA ANATENDWA SANA BAADA YA KUMSAIDIA MWANAMKE
Tukio linakuwa kama ifuatavyo
utasikia Mwanamke ametelekezwa na ujauzito au watoto kisha analalamika kupitia manyanyaso baada ya muda anajitokeza mwanaume mpole , mwenye huruma kupitiliza,mwenye kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa haraka, uvumilivu uliopitiliza na ustaarabu sana,Unakuta mwanaume huyo anajitoa mhanga kifedha kumhudumia mwanamke ambaye ametelekezwa na ujauzito au watoto.
Hapo mwanaume anakuta Mwanamke hana kazi,hana elimu,hana uelekeo wowote,hana ndugu wala marafiki kisha mwanaume anajitoa mhanga kusomesha watoto wa mwanaume mwenzake ambaye yupo busy kunywa pombe na kubadilisha wanawake kama nguo.
mwanaume anahudumia Mwanamke na watoto , atamjengea, atamsomesha atamfungulia biashara,atahudumia ndugu wa Mwanamke huyo alitelekezwa na ujauzito au watoto.
Baada ya siku au miaka kupita yule baba wa mtoto aliyemtelekeza na ujauzito au watoto anakuja kuomba msamaha,anapiga magoti,anatishia kujiua,atadai amebadilika kisha Mwanamke alitelekezwa na ujauzito au watoto anamsamehe na kuamua kurejesha mahusiano kama zamani na mzazi mwenzie.
Baada ya siku kadhaa Mwanamke huyo alitelekezwa na ujauzito au watoto anatafuta kisingizio cha kuibua ugomvi kisha atamdhalilisha mwanaume wake aliyejitoa mhanga kubadilisha maisha ya Mwanamke huyo.
Kisha Mwanamke huyo anarudiana na mzazi mwenziye,baada ya siku kadhaa anapewa ujauzito kisha anafukuzwa kwa mara ya pili,kisha Mwanamke huyohuyo anarudi kuomba msamaha kwa yule mwanaume ambaye alijitoa mhanga kumfariji na kubadilisha maisha yake.
Matukio kama haya husababisha wanaume wengi kuwachukia Single mother.Je nini cha kufanya kukabiliana na hali kama hiyo ? kupitia ndani ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI ukurasa wa 103-125 utakuta maelezo kwa kirefu.
mfano wa pili.
2.MWANAMKE MWENYE HURUMA KUPITILIZA ANATENDWA SANA BAADA YA KUJITOA MHANGA KUBADILISHA MAISHA YA MWANAUME
Mwanamke anakuwa mwenye huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu na kujitoa mhanga.
Anakutana na mwanaume ambaye hana kazi wala biashara yoyote.
Mwanamke anakubali kulala chini,kuvaa nguo za kupauka,anafanya kazi ngumu sana ,anakosa chakula na matunzo akiamini siku mwanaume akifanikiwa kusimama vizuri kiuchumi watakuwa na familia nzuri sana.
Kwa neema za Mwenyezi Mungu riziki inafunguka mwanaume anasimama vizuri sana kiuchumi,hapo anakuwa na maduka,vyombo vya usafirishaji,nyumba ,viwanja kadhaa.
Chimbuko la mafanikio hayo makubwa ya kiuchumi kuna Mwanamke mpambanaji ambaye amejitoa mhanga kupigana na hali ngumu ya kimaisha.
Baada ya mwanaume kuona amekuwa na mafanikio makubwa sana ya kiuchumi,anaanza kumtukana, kumkashifu, kumkaripia kumgombeza, kumtangaza vibaya, kumdhalilisha, kumuingilia kinguvu,au anadai Mwanamke wake ni mchafu sana anatoa harufu mbaya sehemu za siri.
Mwanaume anaanza kubadilisha wanawake kila siku,anamfukuza Mwanamke wake wa enzi za ujana.Baada ya mwanaume kupata Mwanamke wa hadhi yake , biashara zote zinakufa,mwanaume anarudi kufikisika kama zamani.
Kisha mwanaume hiyohiyo anajifanya kwenda kuomba msamaha kwa Mwanamke wake wa enzi za ujana,kisha anamsamehewa kisha anarudia kitendo kilekile.
matukio kama haya husababisha wanawake wengi kuwakataa wanaume ambao hawajasimama vizuri kiuchumi kwa kuhofia kuachwa mpweke baada ya mwanaume kusimama vizuri kiuchumi.
Nini cha kufanya kuepuka aina hizi mbili za matukio?
twende pamoja kupitia summary ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI.
MAKOSA YA KUEPUKA ILI USIJE KUUMIZWA KWENYE MAHUSIANO
Makosa haya 6 kama usipofanyia kazi utalia kilio kikali sana.
1.EPUKA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA SANA KWA MWENZA WAKO
Fanya uwekezaji mkubwa sana kwako siyo kwa mwenza wako.
epuka kumsomesha mwenza wako kama wewe haujaenda shule,epuka kumfungulia mwenza wako biashara kama wewe hauna biashara,epuka kumnunulia zawadi za gharama mwenza wako kama iPhone wakati huohuo unatumia simu ya batani (kiswaswadu/kitochi),epuka kumjengea mwenza wako wakati huohuo hauna hata uwanja,epuka kumnunulia mwenza wako nguo za gharama wakati huohuo wewe unavaa mitumba.
Kosa hili ukifanya utalia sana.
Mwenza wako akiwa na maisha mazuri sana kiuchumi kukuzidi wewe ambaye kwa fedha zako ndio umebadilisha maisha yake tambua kwamba mwenza wako atakuacha ghafla bila kosa lolote atakwenda kwa mtu mwingine kwa madai kwamba wewe sio wa HADHI yake.
2.EPUKA KUJENGA NYUMBA KWENYE UWANJA WA MAMA AU BABA MKWE
epuka kujenga nyumba kwenye kiwanja ulichopewa na mama au baba mkwe mpaka hati ya uwanja iandikwe majina yenu nyote wawili.
Ukijichanganya ukijenga kwa misingi ya kuaminiana atakugeuka ghafla baada ya kuona nyumba imekamilika kwa gharama zako.
Epuka kusomesha watoto wa mwenza wako kama wewe hauna mtoto,epuka kumtafutia kazi mwenza wako kama wewe hauna kazi,
Epuka kujitoa mhanga kwa mwenza wako kama hana shukurani kwako.Kama mwenza wako hana MSAADA wowote kwako acha kujitoa mhanga kwake ,hata akiwa na huzuni epuka kutaka kujitutumua uonekane faraja yake kwa sababu siku ambayo atakuwa mwenye furaha tu atakugeuka ghafla kama vile siyo yule ambaye alikuwa anatia huruma.
3.EPUKA KUTUMIA FEDHA NYINGI SANA KUBORESHA MAISHA YA MWENZA WAKO WAKATI MAISHA YAKO NI MAGUMU SANA
Kosa hili ukifanya utalia sana siku sio nyingi.
Acha kuwekeza fedha nyingi sana kwa mwenza wako badala yake wekeza kwako wewe mwenyewe,kula vizuri, vaa vizuri,tumia manukato yenye harufu nzuri kisha ndiyo uanze kumjali mwenza wako.Hauwezi kuboresha maisha ya mwenza wako wakati wewe umepauka.
mwenza wako akianza kupendeza wakati huohuo wewe umepauka anakuacha ghafla bila sababu zozote za msingi,atatafuta kisingizio cha kuibua ugomvi,atasema wewe sio wa HADHI yake.
Mwenza wako hawezi kuthamini uwekezaji wako kwake bali atathamini uwekezaji wake kwako.
Mwanamke unaweza kumkuta analala chini,anapigwa, anadhalilika,ataingiliwa kinguvu lakini haondoki wakati huohuo wewe ni mwanaume unampa fedha nyingi sana,unanunua zawadi za gharama kubwa sana,unataka kumsaidia awe na maisha mazuri sana lakini utashangaa anakuwa king’ang’anizi sehemu- anapigwa, kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho, vipigo, kugombezwa, kukaripiwa n.k hii ni kwa sababu mwanamke huwa anathamini sana jasho lake siyo jasho la mwanaume.
Mwanamke akifanya uwekezaji mkubwa sana kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume hata kama atamfumania mwanaume huyo haondoki lakini akija mwanaume mwaminifu anamkataa .
Jasho la Mwanamke ndilo hubeba hisia zake za mapenzi.
Vilevile ukiona mwanaume anakuwa king’ang’anizi ujue amefanya uwekezaji mkubwa sana hivyo anaogopa kupoteza jasho lake.
Mwanamke anaelazimisha mahusiano kuvunjika huwa hajafanya uwekezaji wowote kwenye mahusiano hayo.
Mwanaume ambaye anaelazimisha mahusiano kuvunjika huwa hajafanya uwekezaji mkubwa kwenye mahusiano hayo hivyo hana cha kupoteza.
4.EPUKA KUSOMESHA WATOTO NA NDUGU WA MWENZA WAKO IKIWA HAUNA WATOTO WALA NDUGU ZAKO HAWAJASOMA
Epuka kusomesha watoto na ndugu wa mwenza wako kama wewe hauna mtoto wala ndugu zako hawajasoma.
Epuka kuwajengea ndugu wa mwenza wako kama ndugu zako hawana nyumba ya kisasa,epuka kufungua biashara kwa ajili ya ndugu wa mwenza wako kama ndugu zako hawana biashara.
Ukifanya uwekezaji mkubwa sana wakati huohuo mwenza wako anakula bure,anavaa bure,hana kazi yoyote wala hana MSAADA wowote kwako moja kwa moja mwenza wako ataanza kuonyesha dharau waziwazi,atakusaliti waziwazi,atakujibu vibaya,atatoroka kwenda nyumbani kwao mara kwa mara,atabeba ujauzito wa mwanaume mwengine,atakunyima unyumba kwa makusudi,atatishia muachane mara kwa mara kwa sababu yeye hana cha kupoteza,hajatoa jasho
lolote kwa ajili yako.
Wewe utakuwa king’ang’anizi kwa sababu ya kuogopa kupoteza uwekezaji wako na jasho lako ambalo umewekeza kwake.
5.EPUKA KUTAKA KUBADILISHA TABIA YA MWENZA WAKO
Epuka kutaka kubadilisha tabia ya mwenza wako,kama mwenza wako akiwa na tabia ambazo hauwezi kuzikubali mwambie abadilike na ikiwa hawezi muachane.
mwenza wako atakuwa na kiburi, majivuno, jeuri na dharau kwa sababu anakuona hauna furaha bila yeye,mara kwa mara anakuona unampa ushauri, kumbembeleza, kumkumbusha wema umefanya zamani,
kutokana na hali hiyo utaona mwenza wako anakuwa mkali kupitiliza, anakuwa mbabe,anakuwa haambiliki, anakuwa mjuaji sana,anakuwa hashauriki anakuwa hataki kuambiwa makosa yake, hataki kukosolewa, hataki kupewa maagizo,hataki kurekebishwa tabia.
kwanini anakuwa hivyo ni kwa sababu anafanya uzembe kwa makusudi,anafanya makosa kwa makusudi kabisa kisha anageuza kibao kwako,anakuwa na matumizi mabovu sana ya fedha kwa sababu anakukomoa,
Anajua akifanya makosa unasamehe,anajua akiharibu kitu chochote utafanya matengenezo,anajua upo na uvumilivu uliopitiliza,anajua upo na huruma kupitiliza hivyo anajua hauna madhara kwake hata akifanya makosa makubwa sana.
Kadiri unavyotaka kubadilisha tabia ya mwenza wako ndipo utakuwa na wakati mgumu sana kumtoa kichwani endapo mtaachana.Lakini yeye atakuwa na wepesi kukutoa kichwani kwa sababu hajafanya uwekezaji wowote kwako.
6.EPUKA KUVUMILIA TABIA ZISIZOFAA KUTOKA KWA MWENZA WAKO
Epuka kuvumilia tabia kama kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho, vipigo, kugombezwa, kukaripiwa, kutolewa dosari za muonekano,
kadiri unavyotaka kubadilisha tabia ya mwenza wako ndipo utagundua kwamba hauna furaha yoyote, vilevile akija mtu ambaye anakupenda sana na kukuheshimu utakuwa hauna hisia zozote kwake kwa sababu akili yako inafikiria sana uwekezaji wako. Makala hii imeandaliwa na Abdallah Zalala.
