Wananchi wawaosha KenGold Six O’clock

Na John Marwa


Mabingwa watetezi Young Africans wamechakaza KenGold kutoka chunya jijini Mbeya mabao 6-1 mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL) 2024/25 katika Dimba la KMC Co

Yanga waliingia kwenye mchezo huo wakiwa wameagana na Kocha wao Mkuu Sead Ramovic ambaye mkataba wake ulifikia kikomo jana baada ya pande zote mbili kukubaliana kuacahana.

Mabao ya Yanga yamewekwa kambani na Prince Dube akifunga mabao 2, Clement Mzinze mabao 2, Pacome Zouzoua na Duke Abuya wakifunga bao moja moja.


Wananchi waliweka shinikizo wenye mpira kwa idadi kubwa ya wachezaji pale KenGold wakiwa na umiliki wa mpira huku wakifunga njia za pasi, kukamba kaunzia mstari wa kwanza wa ulinzi.

Lakini pia Yanga walikuwa na uraka sana wa kurejesha mpira kwenye umiliki wao na kutengeneza nafasi za kufunga na kufunga mabao kuliko kukaa na mpira muda mwingi.


Baada ya hapo ilikuwa tu ni kesi ya kwamba Yanga wanataka kufunga magoli mangapi na wafungaji wawe wakina nani.! KenGold walizidiws kila kitu uwanjani.

Kipigo hicho kwa KenGold ni kama walistahili na zaidi kwani ndio timu iliyofanya usajili zaidi ya wachezaji 15 kwenye dirisha dogo la usajili ambapo ni sawa na timu mpya kuanza kujengwa bila kuwa na muda wa kutosha wa maandalizi.


Ushindi huo unawafanya Yanga kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi wakifikisha pointi 45 michezo 17 huku nafasi ya pili ni mtani wao Simba SC wenye pointi 43 michezo 16 ambapo kesho watashuka dimbani kuzisaka alama tatu za kuwajesha kileleni dhidi ya Fountain Gate FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *