BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), limemthibitisha John Mnyika kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, huku Amani Kolubwa, ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, akiteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara.

Mapema leo, baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lisu alisema anaanza kazi mara moja na kwamba atamteua Katibu Mkuu na kupeleka jina lake kwa Baraza kwa uthibitisho, tayari kwa majukumu yaliyo mbele yao.
Kolubwa ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni wa Tundu Lisu, amechukua nafasi ya Benson Kigaila aliyeondolewa katika nafasi hiyo, huku Wakili Ali Ibrahim Juma, akiteuliwa na kuthibitishwa na Baraza hilo kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, kuchukua nafasi ya Salim Mwalimu, aliyepewa mkono wa kwaheri.
Akizungumzia uteuzi wake huo, Tundu Lisu aliyemng’oa Freeman Mbowe katika nafasi aliyohudumu kwa miaka 20, alisema Mnyika ni mmoja wa wafanyakazi waadilifu ndani ya Chama hicho, anayepaswa kubaki kukipigania chama.
Wajumbe watatu wa Baraza Kuu Chadema walipinga uteuzi wa Mnyika, lakini Tundu Lisu akatumia Itifaki ya wengi wape, ambapo aliridhia uthibitisho wao kwa Mtendaji Mkuu huyo wa Chama, ambaye wakati wa kinyang’anyiro hiki, hakujichagulia upande kama walivyofanya Wana Chadema wengine walio nje ya Sekretarieti,