Wananchi wahimizwa kufuatilia Vitambulisho vya Taifa

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo amewaasa na kuwahimiza wananchi  kufuatilia vitambulisho vyao vya Taifa mara baada ya kujisajili ili kuepuka changamoto mbalimbali zinazojitokeza wanapohitaji huduma muhimu za kijamii

Mhe Sillo amezungumza hayo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) sambamba na kuzungumza na watumishi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Sillo, ameeleza kuwa vitambulisho zaidi ya milioni 20 tayari vimetengenezwa na kupelekwa Ofisi husika lakini bado kuna changamoto ya baadhi ya watu kushindwa kufuatilia vitambulisho hivyo kwa wakati

Kadhalika Naibu Waziri alimpongeza Mkurugenzi wa NIDA na Watumishi hao kwa kazi kubwa wanayoifanya ya  kuhakikisha huduma ya Vitambulisho inawafikia wananchi pamoja na ongezeko la uzalishaji wa vitambulisho hivyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) James Kaji amesema kuwa mamlaka hiyo imeanzisha mfumo wa kutuma jumbe za simu kwa wananchi ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho ambapo tangu walipoanza tuma ujumbe wa simu ndani ya masaa 24 pekee vitambulisho zaidi ya laki  400,000 vimechukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *