RUVUMA MGUU SAWA UBORESHAJI WA DAFTARI, WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA

MAAFISA Waandikishaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma zinazotaraji kuanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Jumapili ijayo ya Januari 12 hadi 18 kwa muda wa siku Saba kila kituo, wamesema maandalizi ya uboreshaji huo yamekamilika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayonetriki, maafisa hao watoa wito kwa watendaji hao wa vituoni kutunza vifaa na kuwa na ushirikiano huku pia wakikiri kupokea vifaa kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya zoezi hilo.

Nao Maafsa Waandikishaji wasaidizi kutoka Kata za Tanga, Lizaboni na Misufini wametoa wito kwa wananchi wenye sifa kujitokeza kujiandikisha.

Mikoa ya Ruvuma, Njombe, Rukwa na Songwe itahusika kwa uboreshaji huu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoanza Jumapili hii ya Januari 12 hadi 18, 2025 kwa muda wa siku Saba kwa kila kituo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *