Rais Dk. Mwinyi: Ongezeko la Wawekezaji Sekta ya Utalii linachangia Ukuaji wa Uchumi

MUONEKANO wa Majengo ya Mradi wa Hoteli ya SSPD –Buhairan –Planhotel SA, inayojengwa Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja, iliyowekwa Jiwe la Msingi la ujenzi wake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi leo 6-1-2025, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Hoteli ya SSPD – Buhairan-Plan Hotel SA inayojengwa Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja leo 6-1-2025, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Ayuob Mohammed Mahmoud na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Said Ahmed. (Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakipata maelezo ya Mradi wa ujenzi wa Hoteli ya SSPD- Buhairan-Plan Hotel SA, inayojengwa Bwejuu kutoka kwa Meneja Mradi huo Bahaaedin Abdelmonem, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Hoteli hiyo uliofanyika leo 6-1-2025, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Na Mwandishi Maalum

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa kuna  Ongezeko kubwa la Wawekezaji katika Sekta ya Utalii hatua inayochangia Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya nchi.

Amebainisha kuwa Ongezeko hilo la Wawekezaji pia linachangia Ongezeko la Watalii wanaotembelea  nchini hali inayoiimarisha sekta ya Utalii.

Rais Dk, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipoweka Jiwe la Msingi la  Ujenzi wa Hoteli ya  SSPD-BUHAIRAN  iliyopo  Bwejuu Mkoa Kusini Unguja Inayomilikiwa na Wawekezaji kutoka Falme  za Kiarabu.

Rais Dk, Mwinyi amefahamisha Kuwa Faida za Utalii ni Kubwa kwa nchi  katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kuwahimiza  Wananchi kuendelea Kuwaunga Mkono Wawekezaji wanaowekeza maeneo mbalimbali.

Amezitaja Faida hizo kuwa ni pamoja  na Fursa za Ajira kwa Vijana  zile moja kwa moja na nyengine  zisizo za moja kwa moja , Upatikanaji wa soķo kwa bidhaa zinazozalishwa na  Wakulima  na  Wavuvi kwa bidhaa za Baharini na Ongezeko la Pato la Taifa.

Akizungumzia Uwekezaji wa Hotel hiyo aliyoielezea kuwa ya Viwango Rais Dk. Mwinyi  ameeleza  kufunguliwa kwake kutafungua Milango kwa Zanzibar kupokea Wageni wengi zaidi kutoka Falme za  Kiarabu.

Aidha amewapongeza Wananchi wa Bwejuu na Mkoa wa Kusini kwa Kuonesha Utayari wao  na Kuwakaribisha  Wawekezaji hao.

Wakati huohuo Rais Dk Mwinyi ameridhia Ombi lililowasilishwa na  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhammed  Mahmoud  kwa niaba ya Wananchi la kutengenezewa Barabara Ya Kilomita Tatu  kwa Kiwango cha lami  Kutoka Michamvi Mashariki  hadi Michamvi Magharibi.

Akizungumza katika hafla  hiyo kwa niaba ya Mmiliki na  Muekezaji wa Mradi huo Dk, Muhammed Omar ameishukuru Serikali kwa  kukubaliwa kuwekeza Mradi huo aliouelezea kuwa Utawanufaisha   Wakaazi wa eneo hilo kwa Fursa za  ajira 500 pamoja na kuchangia Uchumi wa nchi.

Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya  Uwekezaji  Zanzibar ( ZIPA) Saleh Saad Muhammed amefahamisha kuwa katika Kipindi cha Miaka minne ya Awamu  ya nane  ZIPA imesajili  zaidi ya  Miradi  ya Uwekezaji 430   ikiwa na thamani ya takriban Shillingi Bilioni 5.6  itakayotoa fursa za ajira 25,000.

Ufunguzi wa Mradi huo ni miongoni mwa Shamrashamra za Sherehe za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanziibar.

IDARA YA MAWASILIANO – IKULU ZANZIBAR

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *