TUFANYEKAZI KWA UMOJA NA MSHIKAMANO KWA KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU

Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP Akama Shaaban akizungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali katika ukumbi wa Polisi Vwawa Wilaya ya Mbozi Songwe.

Wakaguzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe wakisiliza maelekezo kwenye kikao cha ACP Akama.

Wakaguzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe wakisiliza maelekezo kwenye kikao cha ACP Akama.

Na Issa Mwadangala

Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban amewataka Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali Wilaya ya Mbozi kufanya kazi kwa umoja na kushirikiana kwenye mambo kadha wa kadha hususani katika masuala ya Jamii na kuzuia uhalifu na wahalifu ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia haki za binadamu.

ACP Akama aliyasema hayo Disemba 17, 2024 na kuwataka askari hao Wilayani humo kuendeleza umoja na kufanyakazi kwa ushirikiano pamoja na kuwahudumia wananichi kwa kuzingatia haki zao katika majukumu ya kila siku ya kulinda raia na mali zao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbozi Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Cosmas Mboya amesema ustadi wa askari unapimwa kwa nidhamu na weledi hivyo ni vema kuendelea kujikita katika kutoa huduma bora kwa wananchi ili wananchi waendelee kuliamini Jeshi letu na kutupa taarifa za uhalifu, wahalifu na ukatili wa kijinsia ili kupunguza matendo hayo katika jamii.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea kutimiza jukumu mama la kulinda raia na mali zao kwa kuendelea kufanya Operesheni, Misako na Doria ikiwa ni sambamba na kuzitumia taarifa fiche ili kuweza kuzuia uhalifu na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *