Prof. Tibaijuka: Prof. Janabi anatosha kumrithi Ndugulile WHO, lakini….

BAADA ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kumtaka Prof. Mohamed Janabi kujiandaa na kinyang’anyiro cha kurithi nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO – Kanda ya Afrika) iliyoachwa wazi baada ya Mkurugenzi Mteule Dk. Faustine Ndugulile kufariki dunia, Profesa Anna Tibaijuka ameeleza mfumo unaotumika kujaza nafasi hiyo huku akikiri kwamba chaguo la Rais Samia linakidhi vigezo, lakini kila chaguzi zina siasa zake.

Desemba 10, akiwaapisha viongozi na mawaziri katika Ikulu Ndogo ya Tunguu Zanzibar, Rais Samia aliyemteua Prof. Janabi kuwa Mshauri wa Rais wa Masuala ya Afya, alimtaka pia kujiandaa kugombea nafasi hiyo, ingawa ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Akitumia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Prof. Tibaijuka amekiri kupokea simu nnyingi zinazomtaka kueleza namna nafasi ya Ndugulile inavyojazwa, na kueleza, kwa mujibu wa taratibu za WHO, mchakato wa uchaguzi kumpata mbadala wa marehemu Ndugulile utaanza upya, kwani Shirika hilo halina mfumo wa kumpa nafasi mgombea aliyefuata kwa kura nyingi wakati wa mchakato wa awali.

DAR ES SALAAM/TANZANIA, 7MAY10 – Anna Tibaijuka (Undersecretary-General and Executive Director, UN-HABITAT, Kenya) at the World Economic Forum on Africa 2010 held in Dar es Salaam, Tanzania, May 7, 2010.

“Wengi mmenipigia simu kuniuliza jambo hili. Ninaamini mchakato wa uchaguzi utaanza upya, kwani WHO haina utaratibu wa kumteua aliyekuwa amemfuata Mteule kwa kura za kushika nafasi hiyo.

“Aidha, hakuna utaratibu kwamba mbadala anatakiwa kutoka katika nchi yake, ingawa Executive Bord ya WHO, inaweza kuamua vinginevyo.

“Kinyang’anyiro kikirudiwa nina imani Tanzania itakuwa na haki ya kuteua mgombea mwingine wa kuwania nafasi hiyo upya na ushindi unaweza kupatikana. Hakuna shaka Prof. Janabi anatosha, ila kila uchaguzi una siasa zake.

“Sympathy vote’ (yaani Kura za Huruma) inaweza kutubeba (kama Taifa) au kutubwaga. Ni kusubiri tuone. Apunzike kwa amani Dk. Ndugulile katuachia majonzi makubwa,” ameeleza Profe. Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT) kati ya 2010 hadi 2016.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *