The Dreams Foundation Events yatoa Mafunzo ya Ujasiriamali

Na Hussein Ndubikle

Taasisi ya The Dreams Foundation Events  imetoa Mafunzo ya ujasiriamali kwa akina mama, baba na vijana rika wa Kata ya Yombo wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza jana wakati wa ufungunzi wa Mafunzo hayo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Temeke Lawama Mikidadi alimpongeza Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Hadia Akida kwa kuandaa Mafunzo hayo.

Alisema Mafunzo hayo ni muhimu sana ambapo ameeleza kuwa alichofanya Hadia ni sehemu ya lengo la UWT la kutaka kumuinua kiuchumi mwanamke na kwamba ili mwanamke awe imara ni lazima awe imara kiuchumi.

Lawama amewataka wajasiriamali hao kuyafanyia kazi Mafunzo waliyopata na kuwaeleza umuhimu wa kuhakikisha wanalinda mitaji yao badala ya kuitumia katika matumizi mengine.

“Mtaji ni kitu muhimu, faid ikiwa kubwa unaweza ukaigawa ikawa sehemu ya matumizi ya nyumbani, kusherehekea na Jamii na mambo mengine, lakini sio ule mtaji,” alisema Lawama.

Lawama ameeleza kuwa kuwa wajasiriamali wengi biashara zao hufa Kwa sababu wamekuwa wakitumia mitajii yao kwa ajili ya matumizi mengine.

Ametumia fursa hiyo kuwataka kuunda vikundi vya watu watano watano na kutambua ni jambo gani wanataka kufanya ili iwe rahisi hata kupata mikopo ya Halmashauri ambayo ni asilimia 10 iliyotengwa na Halmashauri Kwa ajili ya Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Amesema kuwa wanafanya mchakato wa wakuhakikisha wanapatia majiko ya Nishati Safi ya Kupikia wajasiriamali hao hususan akina mama na baba lishe, hii ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa The Dreams Foundation Events, Hadia amesema kuwa ameanzisha Taasisi hiyo kwa lengo la kuwasaidia Wanawake, vijana rika, wazee na watu wenye uhitaji ili kuwakwamua kiuchumi.

“Tunawafikia wananchi nyumba kwa nyumba na kuwasikiliza changamoto zao na kujua mahataji yao ili waweze kujikwamua kiuchumi. Hivyo tukaona leo tuwakutanishe wajasiriamali hawa 150 na wadau ili waweze kupata elimu,” alisema Hadia.

Ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau husasan Taifa Gas ambaye ndiye alikuwa mdau Mkuu katika Mafunzo hayo kuwasaidia mitungi ya gesi ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Aidha Hadia ameishukuru Taasisi ya TASACI kwa kujitolea kuwapa elimu wajasiriamali hao wadogo zaidi ya 150 Kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya TASACI Japheth Mswaki amebainisha kuwa moja ya majukumu ya taasisi yake ni kuwawezeha wananchi kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali kupitia vikundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *