Rais Samia awalilia waliokufa kwa ajali Karagwe, aagiza….

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma salam za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kavers, Fatma Mwasa, lutokana na ajali iliyosababisha vifo vya watu saba na majeruhi tisa, huku akitoa maagizo mazito kwa Jeshi la Polisi.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu katika Kijiji cha Kihanga, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, na kupelekea vifo vya watu saba na majeruhi tisa.

“Ninawapa pole familia, ndugu, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Fatma Mwassa, jamaa na marafiki. Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu marehemu wote wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka.

“Nimelielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa madereva wanaongeza umakini na kuzingatia sheria za barabarani hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

“Utekelezaji wa agizo hili uende sambamba na uhuishaji na uwekaji wa alama za barabarani kwenye maeneo hatarishi, pamoja na kuzingatia umbali na maeneo sahihi ya uwekaji wa vituo vya ukaguzi ili vionekane kwa urahisi zaidi.

“Kwa abiria na watumiaji wote wa barabara, nawakumbusha kutumia namba za simu za Makamanda wa Polisi wa Mikoa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, wakati wowote wanapoona viashiria vya uzembe na ukiukwaji wa sheria na alama za barabarani,” imesema taarifa yake kwa umma.
Sababu za kiafya zamrudisha Manula, akwama kwenda Algeria

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mlinda mlango wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Aishi Salum Manula, amepata matatizo ya kiafya namkushindwa kuendelea na msafara wa timu hiyo ulioondoka alfajiri ya leo kwenda Algeria.

Simba ikiwa na wachezaji 22, imeondoka alfajiri ya leo kuelekea Algiers, Algeria, ambako watashuka dimbani Jumapili Desemba 8 kuwavaa CS Constantine katika mechi ya pili Kundi A la Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CL 2024/25).

Kwa mujibu wa taarifa ya Simba, nyanda huyo anayepigania kurejea kikosi cha kwanza, anakokabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Moussa ‘Pinpin’ Camara, ameshindwa kuendelea na safari kutokana na mkwamo wa kiafya, ambao hata hivyo haukufafanuliwa.

“Mlinda mlango Aishi Manula ameshindwa kuendelea na safari baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Algeria tukiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam,” imesema taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *