Mahudhurio ya mashabiki Yanga vs Al Hilal utata mtupu

DAKIKA 15 kabla ya filimbi ya kuanza pambano la kwamba hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL 2024/25), kati ya Yanga na Al Hilal ya Sudan, dimba la Benjamin Mkapa ni kama liko tupu, zaidi ya nusu ya uwanja haijakaliwa.

Ingawa mashabiki bado wanaendelea kuingia uwanjani, lakini hii ni ishara kwamba huu ni muendelezo wa mashabiki wa Yanga kushindwa kujaza uwanja ‘full house’ kama ilivyozoeleka.

Kwa aina ya ubora wa kikosi chao, umuhimu wa mashindano haya, unafuu wa kiingilio cha chini kabisa cha Sh. 3,000 tu, ingetosha kuwa sababu ya kuwasukuma Wana Yanga kumiminika hapa, hata kama ni mchana wa katikati ya wiki.

Lakini kinachoshuhudiwa hapa ni mdororo wa mahudhurio, ambao hauwezi kusemwa kuwa unatokana na matokeo ya mechi mbili za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, wala kutimuliwa kocha wao kipenzi Miguel Gamondi, bali muendelezo wa timu kukosa uungwaji mkono wa mashabiki viwanjani.

Ipo namna uongozi wa Yanga unapaswa kuutafutia dawa mkwamo wa mahudhurio ya mashabiki wao katika mechi zao, lakini mashabiki wanapaswa kujouliza nini hasa wanahitaji kutoka kwa uongozi na mashabiki, wakati wamepewa wachezaji bora, wanaonesha ubora viwanjani na kuwapa Mataji ya ndani kwa misimu mitatu mfululizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *