Benki Kuu yazifungia ‘Application Haramu’ 69 za Mikopo Kidijitali

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imetangaza kuzifungia Programu Tumizi ‘Application’ 69 za mikopo kidijitali zisizo na leseni, ikiwa ni ukiukwaji wa Mwongozo wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Mwaka 2024, unaolenga Uwazi na Ulinzi wa Watumiaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba, wananchi wameonywa kutojihusisha na programu hizo na kwamba Benki Kuu inashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ili kuzifuatilia programu hizo.

Majukwaa na Programu hizo zimeshindwa kukidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024 uliotolewa na BoT Agosti 27, 2024 (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2 Microfinance Service Providers, 2024).

Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.

Kupitia taarifa hiyo, Benki Kuu ya Tanzania imeuarifu umma kwamba Majukwaa na Programu Tumizi ‘Applications’ zifuatazo hazina kibali na haziruhusiwi kuendelea na shughuli za utoaji mikopo kidijitali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *