WAPINZANI wa Yanga katika mechi ya kwanza Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL 2024/25), wameendelea na chambuzi za kimfumo na kimbinu, wakiangazia matokeo ya Mabingwa hao wa Tanzania, siku tano kuelekea pambano baina yao kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Picha na maelezo yanayoonekana kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii yasikutishe, walichojaribu ni kuziangazia mechi 10 walizocheza Yanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara na matokeo yake, ikiwemo vipigo viwili na kutimuliwa kwa kocha Miguel Gamondi na nafasi yake kuchukuliwa na Sead Ramovic, ambaye mechi dhidi ya Wasudan hao itakuwa kibarua chake cha kwanza.
📌عين على خصم الهلال “يانغ آفريكانز” هذا الموسم في الدوري التنزاني:
♦️عدد النقاط 24 نقطة
♦️لعب 10 مباريات :
- فاز في 8
- خسر 2
♦️المرتبه الثانية في ترتيب الدوري بفارق نقطة عن المتصدر سيمبا:
♦️سجل 14 هدف
♦️استقبل 4 أهداف
♦️ثاني اقوي دفاع بعد سيمبا وعزام
♦️خسر آخر مباراتين وتمت إقالة المدرب
♦️لعب في ملعبه 5 مباريات فاز في 3.
♦️لعب خارج ملعبه 5 مباريات فاز في 5.
Kama umepata taabu kukielewa Kiarabu walichotukia, tafsiri ya hayo ni hii hapa chini.
📌Mtazame mpinzani wa Al Hilal, Yanga ya Tanzania
♦️Idadi ya pointi ilizonazo 24
♦️Amecheza mechi 10 za Ligi Kuu
♦️Ameshinda jumla ya mechi 8
♦️Amepoteza mechi 2
♦️Anashika nafasi ya pili, pointi 1 nyuma ya Simba
♦️Amefunga mabao 14
♦️Amefungwa mabao 4
♦️Safu ya Ulinzi imara iliyoruhusu mabao machache nyuma ya Simba na Azam
♦️Amepoteza mechi mbili zilizopita, kocha akafukuzwa
♦️Amecheza mechi 5 nyumbani, alikoshinda 3
♦️Amecheza mechi 5 ugenini na kushinda zote 5