Na John Marwa
Wakati Watanzania wakifurahishwa na kiwango bora cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ walichokionyesha dhidi ya Ethiopia hapo jana katika Dimba la Stade de Martyrs nchini Congo DR na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mambo bado ni magumu kufuzu Afcon 2025.
Licha ya ushindi huo saa chache baadae Guinea walichapa kidude DRC na kufanya mambo kuwa magumu zaidi mchezo wa mwisho wa Stars dhidi ya Guinea Novemba 19 katika Dimba la Benjamin Mkapa ambapo sasa itakuwa ni kufa ama kupona kwa Tanzania.

Swali kubwa wa wahafidhina wa kandanda ni namna ambavyo Guinea ameuimarika baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Stars mzunguko wa pili kisha kushinda mechi tatu mtawalia za kundi H.
Hakuna kingine ambacho Stars ataingia kukitafuta zaidi ya ushindi huku Guinea wao wakihitaji sare ama suluhu kuungana na DRC katika fainali za Afcon 2025 nchini Morocco.
Ni mchezo wa maamuzi unaohitaji ujasiri na roho za maamuzi ikiwa Stars inacheza nyumbani kuna kila namna ya kuhakikisha inatumia vyema uwanja wa nyumbani ili kufanikiwa kuweka rekodi mpya ya kufuzu afcon mara mbili mtawali na mara ya nne katika historia.
Itakuwa heshima kwa Stars kufuzu Afcon 2025 na kuungana na Uganda ambao wamekwisha fuzu ili kuwakilisha mataifaifa hayo waambata wa Makala ya 36 ya Afcon itakayopigwa Afrika Mashariki 2027.
Ni wakati wa watanzania na wana Afrika Mashariki kuicheza hii mechi kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake na kutumia kila silaha halali kimchezo kuhakisha Stars inafuzu chini ya Nahodha Mbwana Ally Samatta.