Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, akifuta chozi alipokuwa akiaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru, kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2024.
Dk. Samia ameongoza waombolezaji mbalimbali kuaga mwili huo wa Mafuru, aliyefariki dunia Novemba 9 mwaka huu wakati akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Apollo, New Delhi nchini India.

Katika Hotuba yake fupi, Rais Samia alikiri kuwa Taifa limepoteza kiongozi imara, mahiri, mbunifu na mzalendo, aliyeshiriki mara kadhaa kushauri masuala mbalimbali ikiwamo miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali.

