Chama cha Sanaa za Ufundi wanawake chaanzishwa


Na Mwandishi Wetu


Umoja wa Wanawake wa Sanaa za Ufundi Tanzania/ Tanzania Women Union of Crafts and Arts (TAWUCA) umeanzishwa chini ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA).
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Tafca, Marco Tibasima malengo ya kuasisiwa kwa chama hicho ni kuwainua wanawake wanaojishughulisha na sanaa za ufundi kimitaji, kimasoko, kielimu, kijamii, kiujuzi na kiufundi.

Tibasima alisema malengo mengine ni kuwapa fursa za mafunzo katika maeneo mbalimbali ya kuboresha sanaa yakiwemo uzalishaji, mikopo nafuu, biashara na masoko.
Aidha Tibasima alitoa wito kwa wanawake kujiunga na chama hicho ikiwa ni sehemu ya fursa kwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *