RC Chalamila aahidi Mil. 15/- Mfuko wa Wasanii Kumuenzi Grace Mapunda

Marehemu Grace Mapunda enzi za uhai wake.

DAR ES SALAAM, TANZANIA

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wasanii mbalimbali kuishi kwa upendo na kutumia vipato vyao kusaidiana wakati wa changamoto za maradhi na sio kufanya misiba ya kifahari, huku akiahidi kutoa Sh. Mil. 15 za kuanzisha wa Mfuko wa Wasanii kumuenzi muigizaji Grace Mapunda, aliyezikwa leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa Hotuba yake ya maziko ya Grace ‘Tessa,’ RC Chalamila alisema kuna haja kubwa ya wasanii wa sanaa nchini wanapaswa kumuenzi mkongwe huyo ambaye ametoa mchango, lakini akaachwa akiteseka bila msaada wowote kutokana sio tu na wenzake kukosa upendo wa kweli, Bali kutokuwa na Mfuko wa Wasanii.

“Tujifunze kutumia pesa zetu kutoka maisha ya watu, tujifunze kutumia pesa zetu kurejesha umojanna amani, tujifunze kutumia pesa zetu kurejesha Nuru na Faraja. Hayo yote yatawezekana pale tu penye umoja, mshikamano baina ya wasanii.

“Nilikuwa nazungumzia na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii, nikamuuliza mna Mfuko wa Wasanii, akajibu tunao, akimaanisha ule wa Rais Samia Suluhu Hassan alioweka pesa za kukopesha wasanii, nikamuuliza mnao mfuko wenu wasanii tofauti na huo, akajibu hawana.

“Sasa kwa niaba ya wenzangu, ofisi yangu itatoa Sh. Milioni 15 za uanzishwaji wa Mfuko huo ili kumuenzi Grace Mapunda ambaye aliipambania Sanaa. Pesa za mfuko huo ambazo najua zotaongezeka, zitumike kusaidia wasanii wakati wa changamoto za maradhi ama vifo.

“Niko tayari kukabidhi ndani ya wiki mbili, Mwenyekiti na Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, kutaneni mpange namna ya kufanikisha hili,” alisema RC Chalamila huku akimpongeza Mchungaji Mwamposa kwa mchango mkubwa aliotoa kupigia maisha ya Grace akiwa anaumwa.

Grace aliaga dunia usiku wa kuamkia Novemba 2, 2024, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam, ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Maziko yake yamefanyika leo yakihudhuriwa na mamia ya wasanii, Viongozi wa Dini na Serikali, kwenye Makaburi ya Kinondoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *