KIBAHA, PWANI
WAFANYAKZI wanne wa Taasisi ya Mikopo ya OYA, wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha leo Oktoba 16, 2024 kwa tuhuma za mauaji ya Juma Said Sefu yaliyofanyika Oktoba 7 Mwaka huu katika maeneo ya Mbagala Mlandizi, mkoani Pwani.
Watuhumiwa wa tukio hilo ni Cristopher John Charlse (23), Emmanuel Joshua (24), Dastan Charles John (23) na Abdallah Felix Wendiliwe (32).

Kutokana na ushahidi wa kesi hiyo iliyosomwa mara ya kwanza kutokamilika, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Emmaeli Lukmani, ameahirisha hadi Oktoba 30 Mwaka huu.
Wafanyakazi hao ambao wamerudishwa rumande baada ya kunyimwa dhamana, wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Monica Mwela mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmaeli Lukumai katika Kesi namba 29566 ya mwaka 2024.