Kanyigo Sekondari ilivyoupiga mwingi

Na Lydia Lugakila, Misenyi

Shule ya Sekondari ya Kanyigo ambayo ni shule ya binafsi inayotoa mafunzo ya Sekondari kwa kidato cha kwanza hadi cha sita kwa Wavulana na Wasichana iliyopo Wilayani Misenyi Mkoani Kagera imetajwa kuupiga mwingi baada ya kuonekana kuwa ya Kihistoria kwa kuzalisha wanafunzi wenye nidhamu na ufaulu Bora ikiwemo maadili ya Dini.

Wakiongea kwa Nyakati tofauti tofauti Wazazi wa Wahitimu Katika mahafali ya 33 ya shule hiyo kwa Mwaka 2024 akiwemo Bi,Namala Lugakila, Jackson Machage na Bi Rukaiya Rushaka walisema tangu watoto wao waanze safari ya kuisaka Elimu wanajivunia nidhamu na maadili kwani wameonyesha mabadiliko sana tofauti na walivyokuja huku wakiwa wameshika sana dini na taalum juu yake.

“Kwangu Mimi naridhishwa na Elimu pamoja na nidhamu ikiwemo maadili waliyopewa Watoto wetu wanaohitimu kwakweli kazi kubwa imefanyika hatuna la kuwalipa Walimu na uongozi mzima wa shule Mwenyezi Mungu ndo atawalipa mmewanoa watoto wetu alisema Bi Rukaiya.

Aliongeza kuwa Katika shule hiyo ana Watoto 4 akiwemo mmojawapo aliyehitimu Mwaka 2023 ambapo alivuna nidhamu na matokeo mazuri kwa kupata nafasi ya kwanza huku akiwawapongeza walimu hao na kuahidi kuchangia shilingi laki 2 ili kuunga mkono suala la Maktaba ya shule.

“Mimi Mwanangu anaitwa Kelly Mwita Machage ambaye ni Muhitimu Mwaka 2024 alikuja shule hapa nikiwa na imani kuwa atakuwa mkakamavu mtiifu na mwenye nidhamu baada ya kupewa taarifa na wenzangu sasa nashuhudia Mwanangu Kelly amekuwa mfano bora kwa shule na kwa jamii kipo alichokivuna hapa KADEA alisema Bi Namala.

Aidha shule hiyo ilianzishwa rasmi mnamo mwezi Januari Mwaka 1985 na umoja wa Wananchi wa Kanyigo , yaani Kanyigo Development Assocation (KADEA) na imeendelea kusifiwa na wazazi wa aina tofauti tofauti waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwaleta watoto wao kupata Elimu huku waliopita shuleni hapo wakiendelea kuwa mfano mzuri kwenye jamii.

Wakisoma risala ya shule hiyo kwa mgeni rasmi moja ya Wahitimu hao akiwemo Denice Mhoja na Komugisha Claire walisema licha ya kujivunia ufaulu mzuri kwa Mwaka uliopita wa 2023 bado nidhamu imeendelea kushika kasi shuleni hapo.

Katika risala hiyo Walisema wanahitimu wakiwa jumla ya Wanafunzi 183 Wavulana wakiwa 83 Wasichana 100 huku mafanikio yao yakiwa ni uvunaji wa nidhamu bora na dini pamoja na ufaulu kwa masomo ya sayansi na sanaa ambapo kwa Mwaka 2023 matokea ya kidato cha nne daraja la kwanza walikuwa Wanafunzi 99 la pili 55 na la tatu wanne huku na wao wakijivunia ufaulu mzuri kwa mtihani wa Taifa wa kidato cha nne Mwaka 2024.

Wahitimu hao Katika lisala yao waliomba nguvu ya pamoja ili kumaliza changamoto ndogo ndogo zilizopo ikiwemo ukosefu wa vioo ya madirisha, ukosefu wa vyanzo mbadala vya umeme hasa wakati wa masomo jambo ambalo hukwamisha zoezi la kujifunza.

“Tunaishukuru Serikali ya China kupitia ubalozi wake hapa Nchini kwa ufadhili wa ujenzi wa Maktaba japo jengo hilo lina ukosefu wa meza na viti, gari la shule tunaomba pia njia mbadala ya kusaidia uzalishaji wa umeme wa uhakika Kama sola itakayotumika umeme ukisumbua au ukikata na uboreshwaji wa huduma za Afya kama kumalizia ujenzi wa Zahanati ya shule.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Katika mahafali hayo Mwemezi Ngemera ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Damax Sulutions yenye makao makuu Dar es salaam alisema yeye ni sehemu ya historia ya shule hiyo kwani tangu kuanzishwa kwake Mwaka 1985 ameshiriki vyema Katika shughuli mbali mbali huku akifaidi matunda ya ufaulu na nidhamu kwa watoto wake ndugu na jamaa zake.

“Nitachangia shilingi laki 5 ili mchakato wa kutengeneza meza na viti uanze na nitaongea na Mkurugenzi Mwenzake kutoka kampuni ya Damax Sulutions kuona namna ya kuunganisha juhudi ya ufadhili wa Wanafunzi watatu kama tulivyofanya kwa Mwaka juzi”alisema Mwemezi.

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Kanyigo Salim Mbaziila aliwapongeza Wazazi wa Wahitimu hao kwa kuiamini shule hiyo huku akiahidi kutowaangusha hata kwa dakika moja Katika suala la taaluma na nidhamu.

“Mimi ninaye wasimamia Wanafunzi kama Mwalimu wa Darasa nafanya hivyo makusudi ili nisiwaangushe Wazazi hivyo kasi yangu ni ile ile” alisema Mbaziila.

Hata hivyo Mbaziila aliwawatakia kheri Wahitimu hao kwa kuwataka kufanya vizuri mtihani wa Taifa ujao na kuwaomba walete matokeo bora pia amewapongeza walimu kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha wanakuwa na Wanafunzi bora shuleni hapo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *