Maafande waliotumwa na Afande wahukumiwa kifungo cha maisha jela

DODOMA, TANZANIA

KESI gumzo ya jinai iliyohusisha ubakaji na kumuingilia kinyume cha maumbile binti mmoja mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam (jina limehifadhiwa), imetolewa jukumu Septemba 30, ambako watuhumiwa wanne walioshiriki unyama huo, kurekodi na kusambaza mitandaoni, wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewatia na hatia waliokuwa watuhumiwa wa kesi hiyo namba 23476 ya mwaka 2024, ambao ni MT 140105 Clinton Damas ‘Nyundo, ‘ ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) na askari wa Jeshi la Magereza C. 1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema.

Sambamba na hukumu hiyo, washtakiwa hao maarifu kwa jina la ‘waliotumwa na Afande, ‘ wametakiwa kumlipa ‘binti wa Yombo Dovya’ kiasi cha Sh. Mil. 1 kila mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *