Simba kusuka au kunyoa CAF CC leo, iko Lupaso vs Al Ahli Tripoli

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC 2024/25), Wekundu wa Msimbazi Simba, leo saa 10 alasiri wanashuka dimbani Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuwavaa Al Ahli Tripoli ya Libya katika mechi ya marudiano, raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

Simba chini ya kocha Fadlu Davis, wanawaalika Al Ahli Tripoli ikihitaji ushindi, ikiwa inahitaji kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya tatu kwa ukubwa ngazi ya klabu Afrika (ikitanguliwa na African Football League (AFL) na CAF Champions League (CAF CL).

Katika mechi ya kwanza jijini Tripoli, Libya, Simba waliwabana mbavu wenyeji wao hao na kwenda nao sare tasa katika dakika 90 zilizoshuhudiwa kiwango bora na cha kuvutia cha Mnyama.

Al Ahli Tripoli watakuwa wakijaribu kusaka sare ya mabao ili kuwatupa nje Wekundu wa Msimbazi, jukumu ambalo linaonekana kuwa gumu, hasa ikizingatiwa Benjamin Mkapa ni dimba la machinjio kwa Simba katika michuano ya CAF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *