
Naibu Spika Wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azan Zungu, akimsikiliza, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, wakati alipotembelea katika Banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya Tamasha la Kariakoo Festival, yanayoendelea katika Viawanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo linalofanyika kwa sikunsaba limedhaminiwa na Benki ya NMB na kushirikisha Wafanyabiashara mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za Serikali Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Sultan.

Naibu Spika Wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azan Zungu, akipokea Tisheti kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Seka Urio, baada ya kutembelea Banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya Tamasha la Kariakoo Festival, yanayoendelea katika Viawanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo linalofanyika kwa siku saba limedhaminiwa na Benki ya NMB na kushirikisha Wafanyabiashara mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za Serikali.
Na Mwandishi Wetu
Naibu Spika na Mbunge wa Ilala, Musa Zungu, amewataka wafanyabiashara wa Kariakoo kujiepusha na hofu ya ushindani na badala yake kuzingatia ubora wa bidhaa wanazouza.
Akizungumza katika maonyesho ya biashara, Naibu Spika Zungu alisisitiza umuhimu wa ubora wa bidhaa kama njia ya kuvutia wateja.
Katika maonyesho hayo, Benki ya NMB ilihudhuria kama mdhamini mkuu, ikitoa elimu kuhusu matumizi ya QR code kwa wafanyabiashara.
Lengo la hatua hii ni kusaidia wafanyabiashara kuepuka kubeba fedha taslimu, ambayo ni hatari. ‘Nawapongeza sana Benki ya NMB kwa kuwa mdhamini wa maonyesho haya na kutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo juu ya jinsi ya kukuza mitaji yao,” alisema Zungu.
Aidha, alizitaka taasisi za umma zinazohusika na wafanyabiashara kutoa elimu katika maonyesho hayo, badala ya kuwa mstari wa mbele katika kukusanya faini.
“Wafanyabiashara hawa ni watiifu na wako tayari kulipa kodi wanachohitaji ni elimu kwanza kabla ya hatua nyingine.”
Naibu Spika, alieleza kwamba baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wamekuwa na hofu wanaposhuhudia kuanzishwa kwa makampuni makubwa na viwanda, wakihisi soko linaweza kupotea.
“Soko la Kariakoo lipo na litadumu (Is there to stay) kinachohitajika ni nyie mmbadiliko chukueni oda mtandaoni na fanyeni malipo kupitia simu. Wakati usafiri wa mtandao ulipoanza kuna baadhi walihisi, biashara zitachukuliwa lakini, biashara inategemea ubora, huduma bora, na mawasiliano mazuri na wateja,” alisema.
Aidha aliwasihi wafanyabishara waendelee kulipa kodi kwa hiari na kutoaa risiti za kieletronic kwa kufanya hivyo inasaidia miaradi mingine kumalizika kama ya mwendokasi na kupunguza misuguani na Mamlaka ya Kodi nchini.
Kwa upande wake, Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam Seka Urio alieleza kuwa wanayo suluhisho la matumizi ya QR code ambayo linasaidia wafanyabiashara kupunguza matumizi ya fedha taslimu.
Alisema mfumo huu unawawezesha wanunuzi kufanya malipo moja kwa moja kutoka kwenye simu zao kwenda kwenye akaunti za benki kwa kufanya hivyo inawapungizia hatari ya kupoteza au kuipiwaa fedha.
Alisema kwa kufanya hivyo bank hiyo inawanigiza katika mifumo mingine, kupunguza gharama za kuhamisha fedha na kuweza kupata mikopo mbalimbali. “Tumefarijika sana kutembelewa na Naibu Spika pia tunatoa hudumz zote za kibank, kama kufungua akaunti na huduma nyingine.”