“Mashabiki wasikate tamaa kwa sababu ndio kwanza ligi imeanza na ndio kwanza mechi mbili na hatujafungwa bali tumetoa sare mbili kwa hiyo naamini bado njia ambayo tumejiwekea tutafikia malengo.
“Kwa hiyo tunaomba tu sapoti yao wasikate tamaa kwa kuwa sisi ndio kwanza tumeanza msimu na bado kuna mechi nyingi sana kwa hiyo sisi sapoti yao tunaihitaji kwa hali ya juu sana naamini wakitupa sapoti yao na sisi tutawafurahisha tukianza na mchezo wa kesho (alhamisi).”
Beki wetu wa kulia, @chilambo20, akitoa neno kwa mashabiki wa Azam FC kwa niaba ya wachezaji wenzake kuelekea mchezo wa kesho Alhamisi dhidi ya KMC.
