“Wanasheria wetu watanzania watofautishe Elimu yao ya sheria zetu za Tanzania na sheria za FIFA, wanapaswa kujua kuna kitu kinaitwa TMS ambayo ilianzishwa na FIFA ili kusiwe na mambo ya double registration…….Yanga Sc wanaweza kuwa na mikataba yao ya halali kama wanavyosema wenyewe ila wanayo kwenye maktaba zao na hawajapeleka TMS, taarifa zao hawajaziingiza kwenye system…..wamekaa nazo taarifa zao hawajaziingiza kwenye sysytem….Mikataba yao haina tofauti na kadi za harusi ” amesema Ismail Aden Rage.
Rage ameyasema hayo leo wakati wa mahojiano na kipindi cha michezo cha Crown Sport kutokana na sakata la Yusuph Kagoma kuchukua sura mpya mara baada ya hapo jana Mkurugenzi wa Sheria wa klabu ya Yanga Simon Patrick kutoka hadharani na mkataba walioingia na Kagoma kabla ya kujiunga na Simba SC.
