TMA yawataka wahandisi kuzingatia huduma za hali ya hewa

Na Mwandishi Wetu

WAHANDISI nchini wamekumbushwa umuhimu wa huduma za hali ya hewa na kuchangia gharama za upatikanaji wa huduma hizo wakati wa utekelezaji wa miradi yao.

Hayo yalizungumzwa na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Hamza Kabelwa, wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa 21 wa Wahandisi uliyojumuisha wahandisi wa ndani na nje ya nchi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 6, 2024.

Dk. Kabelwa alieleza kuwa, katika hotuba ya Waziri wa Fedha ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2024/25, kifungu cha 158 ilijumuisha mapendekezo ya mabadiliko ya kufanya marekebisho ya sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, sura 157 kuhusu Ada za Hali ya hewa kwa usalama wa uendeshaji wa miradi ya ujenzi.

“Lengo la hatua hiyo ni kuongeza mapato yatakayowezesha utoaji wa huduma mahsusi za hali ya hewa ili kuongeza tija na ufanisi wa utendaji kazi na kuimarisha usalama wa watu na mali katika maeneo ya miradi ya ujenzi, ambapo mchakato wa upatikanaji wa huduma hizo unahitaji uwekezaji wa miundombinu ya kisasa na gharama kubwa za uendeshaji,” amesema Dk. Kabelwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *