
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na wa Kati wa Benki ya (CRDB), Muhimuliza Buberwa, akizungumza jijini Dar es Salam leo, wakati wa uzinduzi wa Promosheni mpya kwa kushirikiana na Qatar Airways ambapo wateja wa benki hiyo watakao nunua tiketi kupitia TemboCard watapata punguzo la asilimia 10 kutoka benki hiyo na asilimia 12 kutoka Qatar. (Na Mpiga Picha Wetu)
Na Mwandishi Wetu
Benki ya CRDB leo imezindua promosheni mpya kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Qatar Airways ambapo wateja wa shirika hilo watapata punguzo hadi asilimia 12 kwenye tiketi zao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Promosheni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na Kati, Muhumuliza Buberwa, alisema kuwa “sisi kama benki tutawarudishia asilimia 10 wakifanya malipo ya tiketi zao kupitia TemboCard VISA yoyote ya CRDB hata za Simba na Yanga.
Uzinduzi wa promosheni hiyo umefanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB huku ukishuhudiwa na Mkuu wa Kitengo cha Kadi, Farid Seif, Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi, Stephen Adili pamoja na maafisa kutoka Qatar Airways Julliette Mkonyi, Bhavin Sonegra, Shirley Mahiku, Sia Minja wakiongozwa na Meneja Mkazi Isaac Wambua.

Meneja Mkuu wa Qatar Airways, Issack Wambura, akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ambapo wateja watakao nunua tiketi kwa kutumia TemboCard watapata punguzo la asilimia 12 na punguzo la asilimia 10 kutoka benki ya CRDB.


