NMB yatoa mafunzo kwa Walimu kuujua, kuutumia Mfumo wa ESS

Mkuu wa Divisheni ya Utumishi na Rasilimali Watu Halmashauri ya Mji Kibaha, Protas Dibogo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa walimu yanayotolewa na Benki ya NMB juu ya namna bora ya matumizi ya Mfumo wa Huduma Binafsi kwa Wafanyakazi (ESS) unaowawezesha kuomba na kupokea mikopo toka taasisi za fedha kwa njia ya simu.

Meneja Mwandamizi Idara ya Bima Benki ya NMB, Borondo Chacha, akitoa mada kuhusu masuala ya Bima katika semina walimu “Mwalimu Spesho, Umetufunza Tunakutunza” iliyofanyika katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Meneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi Benki ya NMB, Queen Kinyamagoha, akizungumza na baadhi ya walimu wakati wa akitoa elimu ya utendaji kazi wa Mfumo wa Huduma Binafsi kwa Wafanyakazi (ESS) unaowawezesha kuomba na kupokea mikopo toka taasisi za fedha kwa njia ya simu.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi wa Kisarawe mkoani Pwani, Bertha Mungure, akizungumza na walimu wa shule za msingi na sekondari Wilaya ya Kisarawe wakati wa Warsha ya kutoa elimu kwa kada ya walimu kwenye warsha iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Minaki.

Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kulia), akisalimia na Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Ofisa Elimu Sekondari, Editha Fue, wakati wa Warsha ya Mwalimu Spesho “Umetufunza Tunakutunza”, iliyoandaliwa na benki ya NMB, wilayani ya Kisarawe iliyokuwa ikitoa elimu kwa walimu hao kuhusu kutumia huduma za benki hiyo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Minaki. Kushoto ni Meneja wa Tawi la NMB Kisarawe, Bertha Mungure.

Meneja Mauzo Huduma za Kidigitali Benki ya NMB, Hezbon Mpate, akitoa mada katika mafunzo ya Walimu iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *