
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya vituo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao mbele ya Afisa Mwandikishaji Msaidizi wa Halmashauri hiyo, Charles Kafutila leo tarehe 18 Agosti, 2024. Mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari unaotarajiwa kufanyika kwenye mkoa huo kuanzia tarehe 21 hadi 27 Agosti, 2024 sambamba na mkoa wa Mwanza. (Picha na INEC).
