Na John Marwa
HAKIKA dakika 90 za mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) zimeendelea kuthibitisha ubora wa kikosi cha Yanga SC baada ya kuwanyuka Vital’o ya Burundi kwa mabao 0-4.

Vital’o ndio walikuwa wenyenji wa mtanange huo licha ya kufanyika Tanzania katika Dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Wananchi yamewekwa kimiani na Prince Dube, Clatous Chama, Clement Mzize na Aziz Ki aliyefunga kwa mkwaju penati baada ya kuchezewa madhambi.
Kwa ushindi huo Yanga wametanguliza mguu moja ndani katika mechi za hatua ya kwanza ama mtoano kutinga makundi.
Mechi ya marudiano inatarajiwa kupigwa Agosti 24, 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga ikiwa mwenyeji.